![]() |
Wanachama wa chama cha SWAPO Namibia wakifurahia ushindi. |
Chama cha Ukombozi wa Namibia SWAPO,
kimeshinda kwa zaidi ya asilimia 86 ya kura za uchaguzi wa Rais wa nchi
hiyo. Waziri Mkuu wa sasa Hage Geingob ndiye amechaguliwa kuwa Rais
mpya, huku chama hicho ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru wa nchi
hiyo mwaka 1990, kikiwa kimeshinda viti vingi vya kura za ubunge.
Uchaguzi huo umeelezwa kufanyika kwa ufanisi kwa kutumia vifaa vya kielektroniki.
Ili
kufahamu undani wa hali ya mambo ilivyokuwa, nilizungumza na mkazi wa
mji mkuu wa Namibia Windhoek bwana Mussa Nahimana ambaye ni Mrundi
mwenye kufanya shughuli zake nchini humo. Kwanza nilimuuliza, uchaguzi
huo ulifanyika kwenye mazingira gani kwa kuzingatia masuala ya utulivu
na usalama?
Hata hivyo uchaguzi huo umekuwa tofauti na baadhi ya
chaguzi nyingine za Afrika ambapo mivutano na kususia matokeo ni baadhi
ya mambo ambayo hujitokeza, lakini Namibia walioshindwa na walioshinda
wamekuwa katika sherehe ya pamoja.
source: bbc swahili
No comments:
Post a Comment