![]() |
Basi lililoshambuliwa huko Mandera nchini Kenya |
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini
Kenya limesema kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio lililotokea kwenye
machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Wakazi
wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio
Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo
Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio
hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28
waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika
tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia
mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa
Kenya.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick
Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na
watu wengine wanne wamejeruhiwa.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya
imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake
yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali
na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa
nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya
kigaidi.
No comments:
Post a Comment