welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Thursday, 11 December 2014

HII KALI PUNDA WATUMIWA KUTOA UJUMBE KENYA

Baadhi ya wananchi walishangaa Punda walikuwa wanafanya nini mjini kumbe wanaharakati ndio waliowaleta huko kuonyesha uchovu wao

Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa mji wa Nairobi baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.
Kauli mbiu hio ilitumiwa mashambulizi yalipofanywa dhidi ya wakenya mjini Mandera Kaskazini mwa Kenya ambapo wanaharakati walipiga kambi katika ofisi ya Rais wiki kadhaa zilizopita kulalamikia ukosefu wa usalama.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.

Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori hilo alisema kuwa alilipwa na mtu flani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.
Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema mwanaharakati mmoja huku akiwaskuma Punda hao kutoka kwa Lori.
Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...