![]() |
BAISKELI ILIYOTENGENEZWA KWA MADINI YA DHAHABU |
Ni rahisi sana kwa watu kulalamikia
gharama ya kununua baiskeli wengi wakitaka bei nafuu. Nyingi ya baiskeli
nchini Uingereza huuzwa kwa pauni 1,000 shilingi lakini moja na
arobaini pesa za Kenya.
Kwa wengi nchini humo hizo ni pesa nyingi sana.
Hata
hivyo baikeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu imezinduliwa nchini humo.
Bei yake? Pauni laki mbili na hamsini au milioni 36,250,000 pesa za
kenya. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya la Ferari,
kukufahamisha tu.
Baiskeli hio ambayo ilitengezwa
na kampuni ambayo hutengeza vitu vya kifahari, Goldgenie imetengezwa
kwa dhahabu kutoka kwa mikono na vyuma vyake vyote. Kiwango cha dhahabu
iliyotumiwa ni karati 24.
Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie,
wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo
unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.
Na wakati baiskeli hio inavutia
macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi.
Mkrugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye
barabara.
"baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.''
Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,'' aliongeza kusema mkurugenzi huyo.
Kwa
sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa
utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi
ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako
umeiwacha.
No comments:
Post a Comment