Shrika la Ti limeyaorodhesha mataifa ya Uganda,kenya na Burundi kama yalio na ufisadi mkubwa
![]() |
Baadhi ya fedha zinazotumika na mataifa ya Afrika mashariki. |
Ufisadi nchini Kenya bado uko katika kiwango cha juu licha ya juhudi kukabiliana na swala hilo nyeti.
Kulingana
na ripoti ya shirika la Tranparency International ya mwaka 2013,kenya
imerodheshwa ya 136 kati ya mataifa 177 ikiwa na alama 27 katika kipimo
cha 0-100.
Sufuri ina maanisha kwamba ufisadi umekithiri huku na 100 ikionyesha kwamba taifa hilo halina ufisadi.
Hatahivyo
ni taifa la Burundi lenye ufisadi mkubwa miongoni mwa mataifa ya Afrika
mashariki likifuatiwa na Uganda na baadaye Kenya kulingana na utafiti
huo.
Kulingana na mkurugenzi wa shirika hilo nchini Kenya Samuel Kimeu,Kenya haijabadilika katika nafasi yake tangu mwaka 2012.
Amesema kuwa taasisi za umma zinahitajika kuwa wazi kuhusu maamuzi yao .
Katika afrika mashariki ,ni taifa la Rwanda Pekee ambalo limeonyesha juhudi za kukabiliana na ufisadi.
Rwanda
imeorodheshwa ya 49 ikiwa na alama 54,Ushelisheli iko katika nafasi ya
47 ikiwa na alama 54 na Mauritius ikiwa katika nafasi ya 52 ikiwa na
alama 52 ikitamatisha mataifa matano bora barani Afrika.
Botswana
imesalia kuwa taifa ambalo halina ufisadi barani Afrika likiwa katika
nafasi ya 30 na alama 64 likifuatiwa na Cape Verde ilio katika nafasi ya
41 na alama 58.Baadhi ya mataifa yalio na ufisadi duniani ni
Somali,Sudan,Sudan Kusini Libya na Guinea Bissau.
chanzo:bbc swahili
No comments:
Post a Comment