welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Wednesday, 3 December 2014

Msafara wa UN waponea chupuchupu shambulizi Somalia

Waokoaji katika harakati za kuzima moto
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na uwanja wa ndege.
Takriban watu wanne wameuawa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari karibu na msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
Polisi wanasema kuwa bomu hilo lililipuka wakati msafara huo ulipokuwa unaelekea karibu na barabara iliyoko karibu na uwanja wa ndege mjin humo.
Mlipuko wa pili iliripotiwa kulenga vikosi vya muungano wa Afrika umbali wa kililomita 25 kutoka mjini humo ingawa taarifa bado ni finyu.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
Kundi la Al-Shabab, ambalo limehusishwa na wapiganaji wa al-Qaeda, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Somalia na katika nchi jirani ya Kenya.

Mnamo siku ya Jumanne liliwaua watu 36 mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia.
Hata hivyo bado halijatoa yamko lolote kuhusu shambulizi lililofanywa mjini Mogadishu.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...