NINACHOUGUA
Amesema ugonjwa unaomsumbua ni kansa, anajisaidia katika ndoo na
kubebwa na baba yake baada ya kile alichodai mama yake
kumkimbia.Alisimua jinsi anavyotaabika kama ifuatavyo:
“Mimi ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto watatu, nilizaliwa
bila tatizo lolote, nilipendwa na wazazi wangu hasa mama alikua kipenzi
changu kuliko baba, leo hii mama kanikimbia ninatunzwa na baba ambaye
anateseka kwa ajili yangu, najisikia vibaya anavyohangaika nami wakati
hana kazi.
“Wakati nazaliwa wazazi wangu walikuwa wakiishi Mabibo CCM, Dar,
baada ya kutimiza mwaka mmoja nilianza kutokwa na mabakamabaka miguuni
kisha mwili mzima, utosini kukatokea kidonda baadaye vikaanza kuenea
kichwani,vilianza kutoa funza, baba alinichukua hadi Hospitali ya
Muhimbili, hapo sasa nikiwa na akili na kujijua.
Hajira
Twalib akiwa amelala kitandani. “Kila tulipoenda nilikuwa sipewi
matibabu, nilikuwa naambiwa daktari bingwa hayupo, tulienda kama mara
saba hivi ndani ya miezi minne tukaenda tena lakini jibu likawa ni
lilelile, baba alichukia sana aliomba jalada langu, akalichana mbele ya
wauguzi kwa hasira na kisha tukaondoka, hatukurudi tena Muhimbili.
MSAADA WA JIRANI
“Tulirudi nyumbani, kwa bahati nzuri kuna jirani yetu mmoja alinionea
huruma baada ya kusikia kuwa Muhimbili hawakunipa tiba yoyote wala
vipimo, alimpatia baba shilingi laki moja na nusu ili nipelekwe
Hospitali ya Ocean Road. Tulienda na iliwachukua muda mrefu bila kujua
kinachonisumbua, baadaye waligundua kuwa ni kansa.
“Kulitokea uvimbe kwenye jicho la kulia, nilipigwa x-ray ambayo
ilisababisha jicho kufa kabisa na kwa sasa halifanyi kazi na hili la
kushoto nalo likawa halioni vizuri hadi sasa naona kwa shida tena kwa
vitu vya karibu tu.
“Katika mkono wangu huu wa kushoto kuna kidonda kimetokea, baba
aliambiwa atoe shilingi laki saba na nusu ili nifanyiwe upasuaji lakini
hadi leo hii bado hajapata, hana uwezo kwani hata fedha ya kula inabidi
baba akazunguke akiomba ndipo tupate kula.
SIPEWI DAWA ZOZOTE
“Ikawa tukienda Ocean Road tunapewa vidonge vya panadol tu, wakati
fulani tunakosa fedha kwa ajili ya nauli, ilifikia hatua madaktari
wakatueleza kwamba tukae nyumbani watakuwa wanakuja kunipa huduma lakini
walikuja mara moja hawajarudi tena.
“Nakumbuka siku mama yangu anaondoka na kuchukua vitu vyote vya ndani
na kuniacha bila maji wala chakula, baba alihangaika sana akawa
anasaidiwa vitu kwa kupewa na majirani, kwa hali hii ya mateso makali
sambamba na ugonjwa sitachukua muda mrefu, nitakufa kwa mateso bila
kumuona mama.
source: Global publishe
Duh nimesikitika sana
ReplyDeleteHeaven