![]() |
Bi Joyce Mujuru |
Taarifa kutoka nchini Zimbabwe
zinasema kuwa Rais Robert Mugabe amemfuta kazi makamu wake Joice Mujuru,
kufuatia ushindani wa uongozi katika chama tawala cha ZANU-PF.
Awali Bi Joyce Mujuru, alikanusha madai kuwa yeye ni mfisadi na alihusika na njama ya kutaka kumuua rais Robert Mugabe.
Bi
Mujuru alilaaniwa na Rais Mugabe wiki iliyopita na kuondolewa kutoka
wadhifa wake wa makamu wa rais wa chama tawala cha ZANU-PF wakati wa
kongamano la chama hicho mjini Harare.
Amesema ameendelea kupokea
vitisho na kuwa shirika la habari la serikali limeendelea kuchapisha
habari za uongo za zisizo na msingi dhidi yake.
Ilikuwa wiki nzima
ya tuhuma dhidi ya Bi Mujuru kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali
kwa ushirikiano na mkewe Mugabe, Grace Mugabe, ambaye kwa sasa
ameteuliwa kama afisaa mkuu wa chama cha ZANU-PF.
Wengi walimuona Mujuru mwenye umri wa miaka 59, kama mrithi wa Mugabe.
Katika
hatua yake ya kwanza kujibu tuhuma hizo tangu kuondolewa katika chama,
Mujuru alisema amekuwa akitishiwa sana na watu asio wajua.
Aliongeza
kuwa vyombo vya habari nchini humo vimeendelea kumchafulia jina lake
kwa kuchapisha porojo na taarifa za uongo, dhidi yake.
Alisema
hakuna hjata tone moja la ushahidi limetolewa dhidi yake kuthibitisha
madai anayasingiziwa na kutajwa kuwa msaliti mkubwa.
Madai kuwa alipanga njama ya kumuondoa mamlakani Mugabe, ni ya kipuzi sana.
Rais Mugabe, mwnye umri wa miaka 90, amekua mamlakani tangu Zimbabwe kujipatia uhuru mwaka 1980.
Bi
Mujuru alipambana bega kwa bega na Mugabe mapema miaka ya 1970, dhidi
ya utawala wa kibaguzi na kwa wengi alionekana kama mrithi mtarajiwa wa
Mugabe.
No comments:
Post a Comment