![]() |
Luis Van Gaa |
Mkuu wa manchester united Louis van
Gaal, amepewa ruksa ya kutumia pesa bila ukomo katika kusajili wachezaji
anawataka ili kuimarisha kikosi chake.
Man united wametumia £150
milioni kwa usajili wa wachezaji sita Ander Herrera, Luke Shaw, Marcos
Rojo, Daley Blind, Radamel Falcao,na Angel Di Maria, aliyevunja rekodi
ya usajili nchi uingereza kwa ada ya £59 milioni.
Wakiwa katika
nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu man united wanachangamoto ya
kushiriki michuano ya klabu bigwa ulaya msimu ujao.
Bodi ina imani zaidi kwa kocha wake wa sasa kurejesha bahati old traffold kuliko kocha aliyetimuliwa David Moyes.
Van
gaal amepewa mamlaka ya kuamua hatma ya mabeki Rafael, Phil Jones,
Chris Smalling, Jonny Evans kiungo Anderson mshambuliaji Robin van
Persie,ambao mikataba yao inakwisha miezi 18 ijayo.
Klabu
wanatarajia kuanzisha mazungumzo ya kandarasi ya kipa David De Gea,
ambae kandarasi yake inafika kikomo 2016,pia kumpa ofa ya kandarasi mpya
kiungo Michael Carrick kuendelea kubaki.
No comments:
Post a Comment