Ripoti
kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu
wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa
vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie
Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao

Maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed nchini Niger.
Polisi
wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa
la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanaowarushia mawe.
Polisi
wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa
la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanaowarushia mawe.
Siku
ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya
waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na
kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.BBC
No comments:
Post a Comment