![]() |
Msichana mdogo alieolewa |
Bi harusi wa miaka 14 nchini
Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35
baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za
haruysi yake.
Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za
kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara
mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.
Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.
Shahidi
wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa
msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi
katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru
huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.
Hamziyya
alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke
aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi
zimekithiri.
Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa
fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5
mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.
''Alisema kuwa
panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia
mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u
aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa
sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana
Sani.
Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.
Jaji
Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u
ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa
kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.
Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.
Ushahidi
wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa
Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.
Jirani
ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim
Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho
kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande
vipande vyeusi''aliiambia mahakama.
Alikula vipande vinne vya
madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha
yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea kula.
Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.
Lakini
alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine
watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki kwa ghafla.
Viongozi
wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua
watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya
mauaji.
Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu
mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani
Abacha,kulingana na shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch.
No comments:
Post a Comment