![]() |
Raisi wa Ufaransa Francois Hollande |
Raisi wa Ufaransa Francois Hollande
amewapa somo viongozi wa bara la Afrika,kwamba wanapaswa kujifunza kwa
yale yaliyotokea nchini Burkinafaso na sio kung'ang'ania madarakani.
Kauli
ya raisi Hollande imetoka katika mkutano wa nchi zinazozungumza
kifaransa ,unaofanyika nchini Senegal,na kutolea mfano kwa kile
kilichomkuta na kumuondoa madarakani Blaise Compaore na kutilia mkazo
suala la katiba kuheshimiwa.
Akiipigia chapuo nchi yake ,Raisi
Hollande amesema nchi yake iliepusha umwagikaji wa damu na kumsaidia
Compaore kuokoa jahazi lililokuwa likielekea kuzama.
Maandamano
makubwa yamepangwa kufanyika hivi leo nchini Togo wakati ambapo raisi
Faure Gnassingbe anataka kuibadili katiba ya nchi hiyo ili aendelee
kusalia madarakani.
Kufuatia kitendo hicho, raisi Hollande amesema
kwamba muda wa Ufaransa kuingialia migogoro ya nchi zilizokuwa makoloni
yake umekwisha kilichosalia ni kuona wale wote wanaozungumza kifaransa
nchi zao zinafuata utawala wa kidemkrasia.
No comments:
Post a Comment