![]() |
Watoto wa Obama Sasha na malia.wamekosolwa kwa mavazi yao |
Watoto wa rais wa Marekani Barrack
Obama,Sasha na Malia wameshtumiwa kwa kukosa heshima na afisa mmoja wa
chama cha Republican baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa Shukran.
Elizabeth
Lauten ,ambaye ni mkurugunzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher
alitoa matamshi yake katika mtandao wa facebook ambayo baadaye
yalifutwa.
Baada ya kukosolewa Bi Lauten aliomba msamaha kwa kutoa matamshi hayo ya kukera
Alikua akikosoa sketi fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.
Bi
Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati
waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.
Maandishi yake yalisoma:''Kwa
wapendwa Sasha na Malia:najua kwamba bado muko katika usichana wenu
lakini ninyi ni miongoni mwa familia ya kwanza ya taifa hili, tafadhali
jaribuni kuwa na heshima.Tafadhalini jaribu kuheshimu jukumu mulilopewa.
''Mama yenu na baba yenu hawaheshimu nyadhfa zao kama inavyohitajika na taifa kwa jumla.
kwa
hivyo naona kwamba munakosa ile hadhi ya kuwa kioo cha jamii.Maandishi
hayo yaliendelea na kuwashauri wasichana hao kuonyesha kwamba wanaishi
katika ikulu ya Whitehouse.
Vaeni mavazi ya kuonyesha munahitaji kuheshimiwa sio kama muko katika baa.
No comments:
Post a Comment