![]() |
JEMBE LA CHELSEA DIDIER DROGBA |
Wachezaji wawili wa kilabu ya
Newcastle Moussa Sissoko na Jack Colback wote watashiriki katika mechi
ya leo dhidi ya Chelsea baada kusimamishwa kwa mechi kadhaa.
Favriccio
Coloccini hatahivyo huenda asicheze kutokana na jeraha analoendelea
kuliuguza huku Mike Wiliamson ,Daryl Janmaat na Sammy Ameobi wakiwa
hawajulikani kucheza kutokanana majeraha.
Mshambuliaji ya Chelsea
Diego Coast atacheza baada ya kusimamishwa kwa mechi moja huku mlinzi
Gary Cahil akitarajiwa kucheza baada ya kupona jeraha.
Katika
mechi kati ya Liverpool dhidi ya Sunderland,mkufunzi Brendan Rodgers
lazima aamue iwapo atampumzisha Steve Gerrard kbala ya mechi ya kuwania
ubingwa wa Yuropa siku ya Jumanne ambayo nisharti Liverpool ishinde ili
iweze kufuzu kwa raundi ya muondoano.
Phillip Coutino amepona na Jose Enrique anatarajiwa kuanza kucheza baada ya jereha la mguu la muda mrefu.
Adam Johnson wa Sunderland na Wes Brown wanatarajiwa kurudi uwanjani kufuatia majeraha madogo.
Katika
mchuano baina ya Arsenal la Stoke,wachezaji kadhaa wa Stoke
wanakabiliwa na majeraha ikiwemo Glenn Whelan na Robert Huth wenye
majeraha ya paja.
Vilevile Steve Sidwell,Peter Odemwinge,Victor Moses na Dionatan Texeira wote wana majeraha.
Upande
wa Arsenal Nacho Monreal ana jeraha la kifundo cha mguu,huku Kierran
Gibs akitarajiwa kucheza mahala pake baada ya kupata jereha la kiuno.
Wojciech Szeczesny amepoa jeraha kama hilo na sasa anatarajiwa kurudi katika goli
Koscielny na Yaya Sanogo watajaribiwa ili kuona iwapo wako tayari kucheza.
Katika
mechi kati ya Manchester City na Everton,mlinzi wa Manchester City
Eliakim Mangala atashiriki baada ya kusimamishwa kwa mechi moja katikati
ya wili iliopita.
Aleksander Kolarov na Edin Dzeko wanaweza kurudi baada ya kuuguza jeraha la paja huku Steven Jovetic akipumzishwa.
Upande wa Everton mlinzi Antolin Alcaraz anarudi uwanjani baada ya kukosa mechi sita kutokana na jereha la bega.
No comments:
Post a Comment